1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken azungumza na viongozi wa Armenia na Azerbaijan

29 Aprili 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amezungumza na viongozi wa Armenia na Azerbaijan na kusisitiza kuhusu uungaji mkono wa Marekani kwa makubaliano ya amani kati ya mataifa hayo mawili jirani

https://p.dw.com/p/4fHNa
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza wakati wa mkutano na waandishi habari pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20 mjini New Delhi mnamo Machi 2, 2023
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Olivier Douliery/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imesema kuwa Blinken alizungumza jana na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na kumhimiza kuendeleza juhudi zake za mazungumzo na mwenzake waArmeniahuku akikariri kujitolea kwa nchi hiyo katika kuunga mkono juhudi hizo.

Soma pia:Azerbaijan, Armenia mbioni kufikia makubaliano ya amani

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Aliyev, Blinken pia alipongeza hatua ya kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa mchumi mmoja maarufu wa Azerbaijan ambaye pia ni mwanasiasa wa upinzani aliyekuwa amefungwa tangu Julai mwaka jana akisubiri kesi dhidi yake.

Marekani yasisitiza kuunga mkono mazungumzo ya amani kati ya Armenia na Azerbaijan

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imesema, katika mazungumzo tofauti na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, Blinken alisisitiza uungaji mkono wa Marekani kwa ufanisi wa makubaliano ya amani ya kudumu na ya heshima, lakini haikufafanua siku yalipofanyika mazungumzo hayo.