1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRASILIA: Rais wa Brazil aapishwa

2 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCe1

Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, ameapishwa kwa awamu ya pili madarakani. Katika hotuba yake mbungeni, kiongozi huyo ameahidi kuboresha uchumi wa Brazil ambao umekuwa ukivuta mkia ukilinganishwa na uchumi wa mataifa mengine yanayoinukia.

Rais Lula amewakumbusha wabunge hatasahau anakotoka akiwa na maana alikuwa zamani mtoto maskini wa mkulima.

Alizungumzia pia ongezeko la machafuko mjini Rio De Janeiro. Wiki iliyopita wahalifu waliyachoma moto mabasi kumi na kuvishambulia kwa risasi vituo vya polisi. Watu kumi waliuwawa katika vurugu hizo. Rais Lula alivilinganisha visa hivyo na matendo ya ugaidi.