1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Serbia yakubali kuwa mshirika wa NATO.

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjH

Miaka saba baada ya shirika la kujihami la mataifa ya magharibi NATO kufanya mashambulizi dhidi ya Serbia, nchi hiyo iliyoko katika eneo la Balkan imekuwa moja kati ya nchi nyingine mbili kutia saini makubaliano ya ushirika na NATO kwa ajili ya mpango wa amani. Hii inaonekana kuwa ni hatua ya mwanzo kwa nchi hizo zinazotaka kujiunga na ushirika huo wa kijeshi. Bosnia-Herzegovina na Montenegro pia rasmi zimeingia katika makubaliano na NATO mjini Brussels jana Alhamis. Katibu mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer amezionya Serbia na Bosnia juu ya wajibu wao wa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa wa uhalifu , ikiwa ni pamoja na Ratko Mladic na Radovan Karadzic.