1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Ujerumani yakabidhi urais wa umoja wa Ulaya kwa Ureno.

1 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmt

Ujerumani imemaliza muda wake wa miezi sita ya urais wa umoja wa Ulaya na kukabidhi wadhifa huo kwa Ureno kwa kipindi cha miezi sita iliyobaki ya mwaka huu.

Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika mjini Berlin kati ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mwenzake wa Ureno Luis Amado.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Bernard Kouchner ametoa shukrani zake za dhati kwa niaba ya nchi yake kwa Ujerumani kutokana na utendaji wake ikiwa kama kiongozi wa umoja wa Ulaya katika muda wa nusu mwaka uliopita.

Wakati wa uongozi wake wa urais, Ujerumani iliweza kufanikisha umoja wa Ulaya kupata makubaliano ya punguzo la asilimia 20 la gesi zinazoharibu mazingira ifikapo mwaka 2020 na ilitayarisha msingi wa makubaliano mapya ya kufanya mageuzi katika kundi hilo lenye mataifa 27 wanachama.