1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya wapiga marufuku uagizaji wa bidhaa za wanyama

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbZ

Umoja wa Ulaya umepiga marufuku rasmi uagizaji wa nyama. maziwa na wanyama kutoka Uingereza kufuatia mripuko wa ugonjwa wa midomo na miguu kwa wanyama kusini mwa Uingereza.

Uingereza tayari imepitisha uamuzi wa hiari wa kupiga marufuku usafirishaji nje ya nchi nyama na bidhaa za wanyama mwishoni mwa juma kabla ya uamuzi huo wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya uamuzi ambao umetiliwa mkazo na Waziri Mkuu wa Uingereua Gordon Brown na ambao pia unazuwiya usafirishaji wa mifugo ndani ya nchi.

Wakaguzi wa afya na usalama wa wanyama nchini Uingereza wamesema hawakugunduwa ushahidi wa ukiukaji wa taratibu za usalama wa kibolojia baada ya kuitembelea maabara moja ya utafiti kusini mwa Uingereza ambayo ilitajwa kuwa inaweza kuwa chanzo cha mripuko wa ugonjwa huo.

Wakaguzi huko Surrey wanaendelea na uchunguzi kujuwa nini kilichosababisha mripuko wa ugonjwa huo.