1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya wasitisha mazungumzo na Uturuki.

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCix

Viongozi wa umoja wa Ulaya wamemaliza mkutano wao mjini Brussels wakitoa uungaji mkono wao kwa misingi mipya migumu ya upanuzi wa umoja huo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesisitiza kuwa umoja wa Ulaya hautaki kuzizuwia nchi nyingine kujiunga na umoja huo. Hata hivyo hapo baadaye wanachama wapya wataingizwa katika umoja huo pale tu wanachama wa umoja huo watakaporidhika kuwa mataifa hayo yanaweza kushughulikia masuala ya fedha, kijamii na majukumu mengine yaliyoko katika nchi zinazoomba uanachama. Viongozi hao wa mataifa 25 wamepitisha uamuzi wa kusitisha kwa muda mazungumzo ya kujiunga Uturuki katika umoja huo kutokana na kukataa kwake kufungua bandari na viwanja vya ndege kwa vyombo vya usafiri vya Cyprus ya Ugiriki. Kulikuwa pia na makubaliano kuhusiana na utaratibu mpya kuhusiana na sera za uhamiaji, hata hivyo vipengee vya makubaliano hayo bado havijashughulikiwa. Ujerumani inachukua wadhifa wa urais wa umoja wa Ulaya mwezi Januari na kansela Merkel ameahidi msukumo mkubwa wa kufufua katiba iliyoshindwa ya kundi hilo la mataifa.