1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Muda wa marufuku umeongezwa

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBay

Watalaamu wa wanyama wa Umoja wa Ulaya wameamua kuendeleza marufuku ya uagizaji wa bidhaa za nyama na wanyama walio hai kutoka Uingereza hadi tarehe 25 mwezi huu wa Agosti.

Hatua hiyo imechukukuliwa baada ya kuzuka kisa cha tatu cha ugonjwa wa miguu na midomo huko kusini mwa England.

Uchunguzi umeonyesha kwamba virusi vinavyosababisha ugonjwa wa miguu wa midomo vimetokea katika maabara moja ya utafiti ya mjini Surrey.