1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Waziri mkuu wa Kosovo aitolea mwito Ulaya kutilia bidii uhuru wa jimbo lake

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBje

Waziri mkuu wa Kosovo ameutaka Umoja wa Ulaya kuunga mkono mipango ya kulipatia jimbo hilo uhuru mojakwa moja endapo mazungumzo na Serbia kuhusu suala hilo yatashindwa kuzaa matunda.

Nchi za magharibi kwa sasa zinajaribu kuunda azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa juu ya hatma ya jimbo la Kosovo ambapo imependekezwa muda wa miezi minne ya mazungumzo ya makubaliano na Serbia kuhusu kutoa uhuru wa jimbo hilo.

Hata hivyo Urussi mshirika mkubwa wa Serbia imeashiria kutumia kura yake ya turufu kupinga hatua ya kupewa uhuru jimbo hilo mojakwa moja bila ya ridhaa ya Serbia.