1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUNGE LA UJERUMANI KUPIGA KURA JUU YA MFUKO WA MADENI

Abdu Said Mtullya26 Oktoba 2011

Wabunge wa Ujerumani leo wanatarajiwa kuunga mkono Mfuko wa madeni.

https://p.dw.com/p/12zA6

Wawakilishi wa vyama vya Serikali na vya upande wa upinzani nchini Ujerumani, wanakusudia kusimama pamoja bungeni katika juhudi za kuukabii mgogoro wa madeni barani Ulaya.

Pande mbili hizo zimekubaliana juu ya kupitisha azimio la pamoja likatalouimarisha mfuko wa kuziokolea nchi zinazokabiliwa na madeni. Azimio hilo linalotarijiwa kupitishwa bungeni kwa kura nyingi leo litampa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel nguvu za bunge atakaposhiriki kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya unaofanyika leo mjini Brussels.

Hata hivyo azimio hilo la bunge pia litamwekea mipaka Kansela Merkel katika hatua atakazozichukua. Azimio hilo linahakikisha kwamba Ujerumani itatoa dhamana isiyovuka Euro Bilioni 211 kwa ajili ya Mfuko wa kuziokelea nchi zenye madeni.