1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Umoja wa mataifa ya Kiarabu wataka majeshi ya yote ya kigeni kuondoka Iraq.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM2

Jumuiya ya mataifa ya Kiarabu imetoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweka muda ambao majeshi yote ya kigeni yataondoka kutoka Iraq.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya Kiarabu wanaokutana mjini Cairo , wamesema kuwa muda huo uandikwe katika muswada wa azimio la umoja wa mataifa.

Wakati huo huo wameitaka serikali ya Iraq kuondoa sheria zote ambazo zinaruhusu kupewa upendeleo maalum kwa Washia na Wakurd. Wameongeza kuwa makundi yote ya wanamgambo wa Kishia yanapaswa kuvunjwa.