1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Viongozi wa Israel kukutana na wa Palestina hivi karibuni.

16 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaC

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani ametangaza kuwa atakuwa na mkutano utakaojumuisha pande tatu ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Misr Hosni Mubarak , Rice amesema anafikiri mkutano huo unaweza kuwa ni sehemu ya juhudi za kweli za kuleta amani katika mashariki ya kati katika muda wa miaka sita iliyopita.

Misr imesema kuwa iko tayari kuwa mwenyeji wa mkutano huo, ambao unaweza kufanyika katika muda wa mwezi mmoja.

Rice yuko katika ziara ya eneo la mashariki ya kati yenye lengo la kufufua mpango wa njia kelekea amani unaojulikana kama , road map, ambao umekwama.

Pia alikuwa akitafuta kuungwa mkono katika eneo hilo kwa mpango wa rais George W. Bush wa kuwekwa wanajeshi 21,000 nchini Iraq katika juhudi za kuzima ghasia za kimadhehebu nchini humo.