1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chavez apata maambukizi mapya

5 Machi 2013

Rais wa Venezuela Hugo Chavez ambaye amekuwa akiugua saratani kwa karibu miaka miwili sasa amepata maambukizi mapya ambayo yamemsababishia matatizo ya kupumua na kumuweka katika hali mbaya zaidi kiafya.

https://p.dw.com/p/17qZL
REFILE - QUALITY REPEAT Venezuela's President Hugo Chavez holds a copy of the newspapers as his daughters, Rosa Virginia (R) and Maria watch while recovering from cancer surgery in Havana in this photograph released by the Ministry of Information on February 15, 2013. Venezuela's government published the first pictures of cancer-stricken Chavez since his operation in Cuba more than two months ago, showing him smiling while lying in bed reading a newspaper, flanked by his two daughters. The 58-year-old socialist leader had not been seen in public since the Dec. 11 surgery, his fourth operation in less than 18 months. The government said the photos were taken in Havana on February 14, 2013. REUTERS/Ministry of Information/Handout (VENEZUELA - Tags: POLITICS PROFILE HEALTH) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Venezuela Hugo Chavez im KrankenhausPicha: Reuters

Rais huyo wa Venezuela ambaye wakati mmmoja alikuwa ndiye nguzo kuu ya Amerika kusini sasa amesalia kutumia mirija ili kumsaidia kupumua. Chavez hajaonekana wala kuzungumza hadharani kwa karibu miezi mitatu sasa na hivyo basi kuliacha taifa lake lililo na utajiri mkubwa wa mafuta na kanda hiyo ya Amerika kusini kwa jumla kataika hali ya ati ati.

Waziri wa Habari wa Venezuela Ernesto Villlegas amesema kwenye taarifa iliyosomwa kutoka hospitali alikolazwa rais huyo kuwa Chavez amekumbwa na maambukizi mapya na makali zaidi ambayo yametatiza kupumua kwake.

Taarifa hiyo inawadia wiki mbili baada ya Chavez aliye na umri wa miaka 58 kulazwa katika hospitali ya kijeshi ya Caracas punde tu baada ya kutoka kupokea matibabu nchini Cuba kwa miezi miwiwli alipofanyiwa upasuaji wa nne wa kudhibiti sarartani tangu mwezi Juni mwaka 2011.

Upinzani watilia shaka hali ya Chavez

Kutokuwepo kwa Chavez katika kuendesha serikali ambapo hata hakuweza kuapishwa kwa hatamu yake ya tatu madarakani ya kipindi cha miaka sita ijayo kumeughadhabisha upande wa upinzani ambao unaishutumu serikali kwa kudanganya kuhusu hali yake ya kiafya.

Makamo wa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.
Makamo wa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.Picha: AFP/GettyImages

Mamia ya watu wakiongozwa na upande wa upinzani walijitokeza Jumapili iliyopita kuandamana kutaka kujua ukweli wa mambo kuhusu hali halisi ya rais huyo mwenye ushawishi mkubwa katika kanda hiyo ya Amerika kusini.

Maafisa wa serikali wametoa picha chache tu zikimuonyesha Chavez akiwa amelala kitandani mwake huko Havana akiwa na mabinti wake wawili mnamo tarehe 15 mwezi Februari siku tatu kabla alipokuwa akitarajiwa kurejea nyumbani. Kutokuonekana kwake kwa umma na kimya cha serikali kumezua uvumi kuhusu afya yake.

Makamu wa Rais Nicolas Maduro na maafisa wengine wakuu wa serikali ya Venezuela wamewakashifu vikali upinzani kuhusiana na madai kuwa Chavez huenda amefariki ama yuko karibu kufariki wakisema ni njama ya kuyumbisha taifa hilo.

Raia watakiwa wawe watulivu

Waziri wa Habari Villegas amewataka raia wa taifa hilo kusimama kidete dhidi ya kile alichokitaja vita kutoka nje ya taifa hilo na mafisadi walioko Venezuela ambao wamemtusi,kumkejeli na kumchukia rais wao ambao sasa wanatumia hali yake ya kiafya kujaribu kuleta machafuko.

Waziri wa Habari wa Venezuela, Ernesto Villegas.
Waziri wa Habari wa Venezuela, Ernesto Villegas.Picha: Reuters

Maduro anayeonekana kuwa mrithi wa Chavez amekuwa akitoa taarifa zinazokinzana kuhusu uwezo wa rais huyo kuendesha majukumu yake akiwa hospitalini. Chvez ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 14 sasa,alishindwa kuhudhuria shughuli ya kuapishwa kwake tarehe 10 mwezi Januari na mahakama ya juu nchini humo ikahirisha shughuli hiyo kwa muda usiojulikana

Kabla ya kuelekea Cuba mwezi Desemba, Chavez alimteua Maduro kama mrithi wake kisiasa na kuwahimiza raia wa Venezuela kumchagua iwapo atashindwa kurejelea majukumu yake. Katiba ya taifa hilo inasema kuwa uchaguzi unapaswa kuitishwa katika kipindi cha siku thelathini endapo rais atashindwa kutekeleza majukumu yake.

Mwandishi: Caro Robi/AFP
Mhariri: Mohammed Abdulrahman