1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Rais wa Syria apokea ujumbe kuhusu Darfur

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPJ

Rais Bashar al-Assad wa Syria amepokea ujumbe kutoka kwa rais mwenzake,Omar Beshir wa Sudan. Ujumbe huo umehusika na hali ya mambo katika jimbo la mgogoro la Darfur,magharibi ya Sudan na pia uhusiano wa nchi hizo mbili.Risala hiyo iliwasilishwa na Mustafa Othman Ismail alie mjumbe maalum wa Rais Beshir.Ripoti zinasema,pande hizo mbili zilijadili pia matokeo ya kisiasa ya hivi karibuni katika eneo la Kiarabu na vile vile njia za kuimarisha uhusiano kati ya Syria na Sudan.