1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS : Syria na Irak zimeanzisha uhusiano wa kibalozi

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCk7

Irak na Syria zimeanzisha tena uhusiano wa kibalozi baada ya miaka 24.Bendera za nchi hizo zilipandishwa kwenye majengo ya balozi mjini Damascus na Baghdad.Mabalozi wa nchi hizo mbili wanatazamiwa kutangazwa hivi karibuni.Serikali ya Damascus ilivunja uhusiano wa kibalozi mwaka 1982 kwa kutuhumu kuwa Irak ilisaidia uasi wa chama cha “Udugu wa Kiislamu“ kilichopigwa marufuku nchini Syria.Wakati wa vita vya Iran na Irak,kati ya mwaka 1980 na 1988,Syria ilikuwa upande wa Iran.