1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS:Rais wa Syria ziarani Moscow

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCia

Rais wa Syria Bashar al-Assad anakwenda Urussi leo kukutana na mwenzake Vladmir Putin.

Viongozi hao wawili wanatajariwa kuzungumzia juu ya mizozo nchini Lebanon,Iraq na Palestina.

Mkutano huu unakuja wakati ambapo Urusi anatafuta kujiimarisha katika eneo hilo tete la mashariki ya kati.

Duru zinafahamisha kwamba viongozi hao wawili watajadiliana juu ya mpango wa Umoja wa mataifa wa kuunda mahakama ya kimataifa itakayowashtaki watuhumiwa wa mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri aliyeuwawa Februari mwaka 2005 ambapo Syria imehusishwa na tukio hilo.

Syria imekanusha tuhuma hizo lakini sasa serikali ya Beirut inaishutumu Damascus kwa kuchochea mvutano wa kisiasa nchini Lebanon.