1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DARFUR:Dkt Salim Ahmed Salim kuwashawishi viongozi wa kikabila Darfur

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVe

Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika katika mazungumzo ya kutafuta amani kwenye jimbo la Darfur Dkt Salim Ahmed Salim yuko katika eneo hilo kwa ajili ya mazungumzo ya kuwashawishi viongozi wa kikabila kumaliza mzozo uliochukua miaka kadhaa.

Dkt Salim ambaye yuko kwenye mji wa El Geneina amemtolea mwito Wahid Mohammad Ahmed al Nur kiongozi wa kundi moja la waasi aliyekataa kutia saini makubaliano ya kuleta amani Darfur kujiunga na mazungumzo kwa ajili ya usalama katika eneo la Darfur.

Viongozi wengi wa makundi ya waasi hivi karibuni walikubaliana huko Arusha Tanzania juu ya msimamo mmoja kuelekea mkutano wa kilele wa amani na serikali ya Sudan.

Makubaliano ya mwisho ya amani ya jimbo la Darfur yaliyofikiwa kufuatia mazungumzo mwaka 2006 yalivunjika baada ya viongozi wa makundi mawili kati ya matatu ya waasi kukataa kutia saini.