1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA : Rais wa Bangladesh ajiuzulu

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbW

Rais Iajuddin Ahmed wa Bangalesh amejiuzulu kama kiongozi wa serikali ya mpito na ameahirisha uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 22 mwezi wa Januari.

Akihutubia taifa kwa njia ya televisheni Ahmed pia ametanngaza hali ya hatari nchini humo.Hatua yake hiyo inakuja baada ya mfululizo wa maandamano ya wafuasi wa upinzani ambao wanadai kwamba uchaguzi huo hautokuwa huru wala wa haki.

Nafasi ya Ahmed kama kiongozi wa serikali ya mpito ambayo inawajibika na kuandaa uchaguzi huo itachukuliwa na Hakimu wa Mahkama Kuu Fazlul Haq.

Tarehe mpya ya kufanyika kwa uchaguzi huo haikupangwa.