1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan aahidi kurekebisha makosa baada ya kushindwa

1 Aprili 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameahidi hii leo kurekebisha makosa yoyote yaliopelekea kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi wa manispaa.

https://p.dw.com/p/4eJsu
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan wakihutubia umma baada ya uchaguzi wa manispaa
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan wakihutubia umma baada ya uchaguzi wa manispaaPicha: Emin Sansar/Anadolu/picture alliance

Upinzani nchini Uturuki ulitumia madhila ya kiuchumi na wapiga kura wa Kiislamu wanaohisi kutengwa kama turufu ya kukiangusha chama cha Rais Recep Tayyip Erdogan.

Matokeo yas uchaguzi huo wa manispaaa ya miji na majiji uliofanyika jana Jumapili, yameashiria kushindwa vibaya kwa Erdogan na chama chake cha AKP katika muda wa zaidi ya miaka 20 waliokaa madarakani, na kukipa tena nguvu chama kikuu cha upinzani huku ukimuimarisha meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu kama mpinzani mkuu wa rais.

Soma pia: Erdogan asema Uturuki inaliunga mkono kikamilifu kundi la Hamas

Kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa, chama kikuu cha upinzani cha CHP kilishinda kura ya umma na kikachukua sehemu kubwa ya miji mikubwa, kikipenya kwenye ngome ya AKP katikati mwa Uturuki.

Wachambuzi wanasema wapigakura wamekosa uvumilivu na mzigo wa gharama za maisha zinazochochewa na mfumuko wa bei wa karibu asilimia 70, pamoja na mtindo wa siasa za migawanyiko unaendekezwa na rais Erdogan.