1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa rushwa waiathiri FIFA

24 Julai 2015

Mgogoro wa rushwa unaoikumba FIFA unauathiri mchakato wa shirikisho hilo la kandanda la kimataifa wa kuwatafuta wafadhili wapya wa Kombe la Dunia. FIFA haijasaini mkataba wowote na wafadhili

https://p.dw.com/p/1G4Ld
Russland FIFA Jerome Valcke PK in Samara
Picha: Reuters/M. Zmeyev

Wakati ikilenga kupata karibu mapato ya dola bilioni 6 kutoka kwa Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi, FIFA haijasaini mkataba na wafadhili wowore wapya tangu dimba la mwaka jana nchini Brazil. Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema hakuna makubaliano yoyote yanayoweza kufikiwa kwa sasa hadi pale mustakabali wa FIFA utakapokuwa wazi - baada ya rais mpya kuchukua usukani kutoka kwa Sepp Blatter mwaka ujao. Anasema "Ktakuwa na mkutano, mwezi ujao, Agosti, baina ya washirika wote wakuu wa FIFA, na FIFA. Katika mkutano huu, itakuwa FIFA, na sio tu kitengo cha mauzo lakini pia kitengo chetu cha sheria ili kujadiliana nao. Suala kuu ni kuhakikisha, kutoka upande wao, kuwa mchakato wa awali wa mageuzi, mageuzi yanayoendelea, unapaswa kuwa na lazima ufanyike kupitia tume maalum".

Blatter mit Putin 13.07.2014 in Rio
Urusi itaandaa Kombe la Dunia 2018Picha: picture-alliance/RIA Novosti

Kampuni za Coca-Cola, Visa na McDonald's ni wafadhili wakuu wa FIFA ambao wamelitaka shirikisho hilo kufanya mageuzi muhimu.

Wakati huo huo, Jerome Valcke amesema kuwa ataondoka katika wadhifa wa Katibu mkuu baada ya mrithi wa Blatter kupatikana. Hata hivyo Valcke amesema siyo kwa sababu alifanya makosa yoyote kuhusiana na mzozo ambao umelitikisa shirikisho hilo la kandanda. "Ikiwa ningekuwa rais mpya wa FIFA, ningetaka kuwa na katibu mkuu mpya. Hivyo, ndiyo, yeyote atakayekuwa rais wa FIFA anapaswa kuwa na katibu mkuu mpya kwa sbabau ndiyo uhusiano muhimu katika shirika lolote".

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 54 amekuwa katika wadhifa huo tangu mwaka wa 2007. Kwingineko, uwanja wa michezo wa Luznhniki mjini Moscow ndio utaandaa mchuano wa ufunguzi na fainali ya Kombe la Dunia 2018.

Uwanja wa Zenit mjini Saint Petersburg utaandaa nusu fainali ya kwanza mnamo Julai 10 na mshindi wa nafasi ya tatu mnamo Julai 14

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Iddi Sessanga