1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mashauriano yaendelea vyema kuhusu askrai wa Israil anayeshikiliwa mateka.

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeA

Msemaji wa Hamas amesema kuna dalili za matokeo mazuri katika mashauriano yanayoendelea kuhusu kuachiliwa huru mwanajeshi wa Israel anayeshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa Palestina.

Msemaji huyo hakutoa taarifa zaidi lakini alisema mashauriano hayo yameendelea vyema na huenda askari huyo Gilad Shalit akaachiliwa karibuni baada ya Israil nayo kuwaachilia huru wafungwa wa Kipalestina.

Shalit alitekwa mjini Gaza mwezi Juni hali iliyosababisha Israil kuushambulia ukanda wa Gaza ambapo mamia ya wapalestina waliuawa.