1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Mtaalamu wa kuunda mabomu auwawa.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCw1

Ndege za kijeshi za Israel zimeshambulia na kumuua mtaalamu wa ngazi ya juu wa Hamas ambaye alikuwa akiunda makombora mapema leo , wakati mabuldoza mengi yakianza kuvunja nyumba kaskazini mwa Gaza.

Maafisa wa Palestina wamesema kuwa watu wanne zaidi wameuwawa katika matukio tofauti ndani na nje ya mji wa Beit Hanoun, ikiwa ni pamoja na mtu mmoja ambaye amezikwa katika kifusi cha nyumba yake baada ya kushambuliwa na kifaru.

Wengine waliouwawa ni wapiganaji wa Hamas.

Mashambulio haya mapya yanakuja siku moja baada ya majeshi ya Israel kuuwa watu 19, wengi wao raia , ikiwa ni pamoja na wanawake wawili waliokuwa wamejitolea kama ngao ya kibinadamu na kujiweka kati ya majeshi hayo na wapiganaji waliokuwa wamejificha katika msikiti.

Jeshi la Israel limesema kuwa limefyatua risasi kwa Wapalestina wenye silaha tu, na kwamba operesheni yake katika eneo la Gaza ina lengo la kuwazuwia wapiganaji kurusha makombora dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.