1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mwito wa kuwapa tena Wapalestina msaada wa kimataifa

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmx

Mgombea urais wa chama cha Kisoshalisti nchini Ufaransa,Segolene Royal ametoa mwito wa kuanza kuwapatia tena Wapalestina msaada wa kimataifa. Leo,alipotembelea Ukanda wa Gaza,Bibi Royal alisema,Wapalestina kwa dharura wanahitaji huduma za kijamii zinazofanya kazi.Jumuiya ya kimataifa imesita kutoa sehemu ya misaada kwa Wapalestina kufuatia ushindi wa mwezi Machi wa chama cha Hamas chenye mrengo mkali na ambacho hukataa kuitambua Israel.Bibi Royal alie na miaka 53,anaazimia kuwa kiongozi wa kwanza wa kike nchini Ufaransa.Yeye atakumbana na waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanywa tarehe 22 April mwaka ujao.Rais Jacques Chirac wa Ufaransa alietimia miaka 74 siku ya Jumatano,hatazamiwi kugombea awamu ya tatu.