1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina 5 wameuawa Ukanda wa Gaza

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxy

Hadi Wapalestina 5 wameuawa katika mashambulizi mapya ya vikosi vya angani vya Israel. Mashambulizi hayo yalilenga vituo vya wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.Mapema leo hii makombora ya Israel yalipiga pia nyumba ya mlinzi si mbali na nyumba ya Waziri Mkuu wa Wapalestina Ismail Haniyeh.Na katika mashambulizi yaliofanywa wakati wa usiku,wanajeshi wa Kiisraeli walivamia Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan,na kumkamata waziri mwengine wa Hamas katika serikali ya Wapalestina.Waziri wa nchi,Wafsi Qabha, alichukuliwa kutoka nyumbani kwake.Kwa upande mwingine,wanamgambo wa Kipalestina wameipa Israel muda wa saa 48 kukubali kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.Tangu siku kumi zilizopita,zaidi ya Wapalestina 40 wameuawa katika mashambulizi ya Israel.Vile vile mwanamke wa Kiisraeli ameuawa kwa kombora lililorushwa na wanamgambo wa Kipalestina.