1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Watoto wawili wa Kipalestina wauwawa na jeshi la Israel.

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvk

Majeshi ya Israel yamewapiga risasi na kuwauwa vijana wawili wa Kipalestina karibu na mpaka wa Israel na Gaza.

Shambulio hilo lilitokea karibu na makaazi ya zamani ya walowezi wa Kiyahudi.

Duru za Wapalestina zimesema kuwa vijana hao walikuwa sehemu ya kundi la watoto ambao wamekwenda katika eneo hilo kuogelea.

Jeshi la Israel limedhibitisha kuwa wanajeshi wamewapiga risasi Wapalestina kadha ambao walionekana wakitambaa kuelekea ukuta wa mkapa karibu na mji wa Beit Lahiya.