1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GREENSBURG: Wimbi la vimbunga vipya nchini Marekani

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4G

Nchini Marekani wilaya sita za kati zimekumbwa na wimbi la vimbunga zaidi.Sasa juhudi za uokozi kusini mwa Kansas katika mji wa Greensburg ulioteketezwa na kimbunga kikubwa cha siku ya Ijumaa zinacheleweshwa.Watu 9 waliuawa katika kimbunga hicho baada ya upepo wenye mwendo wa kilomita 400 kwa saa,kuteketeza asilimia 95 ya mji huo. Wasaidizi wamelazimika kusitisha kazi zao kwa sababu ya vimbunga vipya.Rais wa Marekani George W.Bush ametangaza hali ya maafa makubwa katika eneo hilo.Idara inayotabiri hali ya hewa imeonya kuwa hali mbaya ya hewa inatazamiwa katika wilaya za magharibi ya kati nchini humo.