1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GUANTANAMO BAY CUBA:Koran ilikashifiwa wakiri wanajeshi wa Marekani

27 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9j

Jeshi la Marekani limekiri kwamba kumetokea mara tano visa ambapo walinzi na wanaowahoji wafungwa wa jela ya Guantanamo bay walikashifu kuran tukufu wakati.

Lakini kamanda wa jela amesema hakuna ushahidi wa kusadikika uliotolewa kwamba walinzi hao waliitumbukiza chooni Kuran tukufu.

Madai hayo yamefichuliwa katika stakabadhi ya mwaka 2002 ya shirika la upepelezi la marekani FBI :

Madai mengine kama hayo yalichapishwa na gazeti la kila wiki la News Week mapema mwezi huu.lakini baadae wahariri wa gazeti hilo waliifutilia mbali ripoti hiyo na kuzusha ghadhabu na maandamano katika mataifa mengi ya kiislamu.

Marekani hivi sasa inawazuilia jela wafungwa 520 katika jela ya Guntanamo Bay kisiwani Cuba.