1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali isiyo na mwisho ya maguezi ya umoja wa mataifa

Sekione Kitojo22 Septemba 2010

Miaka 13 iliyopita katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan alielezea umuhimu wa kuifanyia taasisi hiyo mageuzi.

https://p.dw.com/p/PJZ5
Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa, Kofi Annan ( Kushoto)alizungumzia kuhusu umuhimu wa kuifanyia mageuzi taasisi hiyo muhimu hapa duniani.Picha: AP

Miaka 13 iliyopita katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan ameelezea umuhimu wa kuifanyia taasisi hiyo mageuzi. Ili taasisi hiyo ya kimataifa iweze kusonga mbele katika karne ya 21, kunahitajika uamuzi utakaoungwa mkono, wa kubadilisha utendaji na uongozi wa taasisi hiyo na majukumu yanayoikabili duniani yaweze kutaribiwa kwa ufanisi. Tangu wakati huo mradi huo wa mageuzi ya umoja wa mataifa , unaendelea. Baadhi imekwisha fanikiwa, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Hususan mageuzi katika baraza la usalama hayajafanikiwa. Mada hii itashughulikiwa pia na mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa mjini New York, ambalo linaanza kikao chake leo Alhamis.

Joseph Deiss raia wa Uswisi amejaribu kulizungumzia suala hilo kutoka katika kiini chake. Rais huyo wa 65 wa baraza kuu la umoja wa mataifa amesema katika ufunguzi kuwa taasisi hiyo ni jukwaa muhimu kwa ajili ya mijadala kuhusiana na masuala ya kidunia, lakini..

Kwa jumla baraza kuu la umoja wa mataifa linaonekana kuwa lisilokuwa na nguvu, kama kilabu ya watu wanaojadili mambo ambayo hayana maana.

Anataka serikali za mataifa wanachama kuuangalia tena umoja wa mataifa kuwa ni sehemu muhimu. Ushindani kwa taasisi hiyo yenye umri wa miaka 65 kwa mfano unatoka kwa kundi la mataifa 20 muhimu yenye viwanda na mataifa yanayoinukia kiuchumi , kama yanavyofahamika , mataifa ya G20, ambayo yamekuwa yakiiongoza dunia kutoka katika mzozo wa kiuchumi.

Umoja wa mataifa tayari umekwisha fanikiwa kufanya baadhi ya mageuzi, anasema William Pace, mkurugenzi wa taasisi ya sera za dunia mjini New York.

Katika mwaka 2005 serikali zimefanikiwa kufanya mageuzi muhimu . Wameidhinisha mkataba wa haki za binadamu ikiwa ni nguzo ya tatu muhimu ya umoja wa mataifa , pamoja na nguzo ya amani na usalama pamoja na maendeleo.

Aina na hatua zilizochukuliwa kuidhinisha mageuzi hayo , anasema Pace kuwa haikuwa rahisi kufanikishwa. Lakini imewezekana kwa mfano kuanzisha hali ya kuwajibika kwa mataifa hayo, kuwalinda raia wao dhidi ya uhalifu wa kivita, mauaji ya halaiki, na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Iliundwa pia kamisheni ya kuimarisha amani. Muda mfupi baadaye ilianzishwa pia taasisi kwa ajili ya wanawake. Na katika wajibu wake wa kuzuwia vita vya tatu vya dunia, umoja wa mataifa umeweza kulitekeleza jukumu hilo kwa mafanikio.

Lakini wakati ikihitajika kufikia makubaliano , taasisi hiyo yenye wanachama 192 imekuwa na kazi ngumu, kwamba msingi wa kufikiwa maamuzi mara kwa mara unakuwa hauko katika hali halisi, wakati wa kuratibiwa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton amesema hapo kabla katika hotuba yake ya msingi mjini Washington kuwa....

Tunaunga mkonmo kwa dhati, mageuzi makubwa , ambayo yanasaidia ujumbe wa kulinda amani wa umoja huo sehemu mbali mbali , kuweza kuweka haraka majeshi yenye vifaa na watu waliopata mafunzo barabara kwa upande wa jeshi na polisi pamoja na ubora wa viongozi pamoja na wataalamu wa kiraia ambao wanahitajika.

Kwa hiyo mageuzi ya umoja wa mataifa yanabaki kuwa kazi ambayo haina mwisho.

Mwandishi : Bergmann, Christina / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman.