1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali mbaya katika mjii mkuu wa Somalia,Mogadishu

5 Juni 2007

Hali katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu inazidi kuwa mbaya, baada ya askari wawili na raia watano hii leo siku moja baada ya Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Ali Mohamed Gedi kunusurika kuuwawa na mtu wa kujitoa mhanga.

https://p.dw.com/p/CHD9
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Ali Mohamed Gedi anusurika kuuwawa.
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Ali Mohamed Gedi anusurika kuuwawa.Picha: AP

Majeshi ya Ethiopia pia yamemuua mtu mmoja aliyekuwa na gari lililojaa milipuko ambaye alikuwa akitaka kujibamiza katika makao makuu ya jeshi hilo.

Aboubakary Liongo alizungumza na mwandishi wa habari wa mjini Mogadishu,Ibrahim Elmi, na kwanza alitaka kujua hali ikoje hivi sasa mjini humo.