1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya hewa na Umoja wa Ulaya

Ramadhan Ali8 Machi 2007

Viongozi wa umoja wa Ulaya wanakutana leo na kesho kama mlivyosikia mjini Brussels na usoni mwa ajenda yao ni jinsi gain kuzuwia zaidi kuchafuka kwa hali ya hewa na mazingira kwa jumla.

https://p.dw.com/p/CHIb
Ulaya unataka kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa
Ulaya unataka kupambana na mabadiliko ya hali ya hewaPicha: DLR

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,anauangalia Umoja wa Ulaya unafaa kushika usukani kulinda hali ya hewa isichafuke zaidi na ndio maana anapigania katika kikao cha jana na leo huko Brussels, maazimio madhubuti ya nishati inayotumika tena “Renewable energy”.

Sasa wamefahamu na wanachukua hatua: picha za karibuni za misiba ya hali ya hewa zinaonesha athjari zake na baada ya miaka mingi kupita ya porojo tupu,wanasiasa sasa wanashindana katika kutoa mashauri na mapendekezo jinsi gain ya kuzuwia kuchafuka zaidi kwa hali ya hewa na mazingira.

Mapendekezo yanayotolewa yanaanzia kupunguza misafa ya ndege ya masafa ya mbali hadi kuacha kutumia globu za taa zinazochafua mazingira.Badala ya kufunga safari ndefu za utalii kwenda Seyschelles ,wende karibu kisiwea cha sylt kiliopo Ujerumani.Majadiliano haya hayasaidii kitu kuikoa sayari yetu isizame kwenye mafuriko.

Kinachotakiwa si wahubiri wa uadilifu bali wanasiasa wenye maarifa na werevu .Pamoja nao hao mi kuwa na sera nafuu za kodi na za nishati.Ni katika sdekta hii ambako wanasiasa w ujerumani wameshindwa.Wanatumia kodi ya mazingira sio kulinda hali ya hewa bali kusaidia misaada ya kwa jamii, wanatoza kodi magari bila kujua magari kwa njia hiyo yanasafiri masafa marefu au mafupi,sana au kidogo.

Hawatozi kodi mafuta ya taa na badala yake wanagharimia kwa kulipia fidia viwanja vya ndege ya mikoa ili kusafiri kwa ndege kuwe nafuu na wakati huo huo wanayatoza magari moshi kodi ya usafi wa mazingira.

Ukweli wa hali ya mambo ni huu:Ujerumani pekee haiwezi kuinusuru dunia ,lakini Ujerumani yaweza kutumia wadhifa wake wa UU na wa kundi la nchi 8 tajiri-G8 ili kutetea kwa nguvu usafi wa mazingirta na hali ya hewa.Kwani juhudi zote hizi zitaleta nafuu kidogo ikiwa wachafunzi wengine wa hali yahewa kama vile Marekani,china,India au hata pia Australia watabebeshwa jukumu la kutunza mazingira.

Kwa ufupi, utunzaji barabara wa hali ya hewa utakuwapo tu pale madola makuu ya sayari hii yatakapotambua athari hasa ya misiba ya hali ya hewa na gharama zake na umuhimu wa kuhimiza matumizi ya nishati inayotumika tena au magari yasiotumia mafuta mengi.

Ujerumani kwa mfano ni mabingwa wa dunia katika kuongoza katika nishati inayoweza kutumika tena na mwaka jana pekee kupitia ufundi wake wa kimazingira imejipatia faida ya Euro bilioni 16 na kutoa nafasi za kazi 170.000 katika sekta hii.

Kwahivyo, usafi wa mazingira na hali ya hewa una manufaa yake tena kwa kila hali.