1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Mwanasiasa wa MDC ajeruhiwa vibaya akiwa safarini

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHV

Mbunge mmoja wa Upinzani nchini Zimbabwe alipigwa na kujeruhiwa vibaya na kundi la watu wanane alipokuwa safarini kuelekea nchini Ubelgiji.Hayo yanatokea siku moja baada ya wanasiasa wenzake kuzuiliwa kufunga safari hadi Afrika Kusini kwa matibabu kwa mujibu wa afisa mmoja wa chama hicho.

Nelson Chamisa msemaji wa chama cha Movement for Democratic Change, MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai alikuwa katika uwanja wa ndege wa Harare kusafiri hadi nchini Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa wabunge kutoka Afrika,Pacific ,Carribean na Umoja wa Ulaya aliposhambuliwa na watu wane.

Bwana Chamisa anapata matibabu katika hospitali ya Harare baada ya kujeruhiwa kwenye jicho na taya.Polisi waliwazuia viongozi wengine wawili wa chama cha MDC Sekai Holland na Grace Kwinje kusafiri hadi Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kupigwa walipozuiliwa na polisi juma moja lililopita kulingana na mwanasheria wao.Rais Mugabe mpaka sasa anashikilia kuwa sheria lazima zidumishwe

Nchi ya Ujerumani iliyo mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya kwa sasa inasema kuwa inatiwa shaka na vitendo hivyo.Aidha inatoa wito kwa serikali ya Zimbabwe kuwaachia huru wanachama wa upinzani wanaozuiliwa.