1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimae Urusi na Ukraine zaafikiana kuhusu mzozo wao wa gesi

Jane Nyingi12 Januari 2009

Hatimae Urusi na Ukraine zimekubali kusitisha mzozo wao kuhusu gesi baada ya Ukraine kutia saini makubaliano ya wachunguzi huru watakaokangua usambazaji gesi asili kutoka Urusi hadi Mataifa ya ulaya bila ya vikwazo

https://p.dw.com/p/GWSK
Waziri mkuu wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) akizungumza na mwenzake wa Ukraine Bi. Yulia Timoshenko (kulia)Picha: picture-alliance/ dpa

Urusi ilikuwa imesimamisha usafirishaji gesi kupitia mabomba ya ukraine,kwa madai kwamba Ukraine ilikuwa inaiba gesi hiyo iliokusudiwa kwenda barani Ulaya.

Makubaliano hayo kati ya Urusi na Ukraine yametoa afueni kwa mataifa kadhaa barani ulaya ambayo tayari yalikuwa yameanza kuathiriwa na mzozo huo.Ni mkutano wa leo asubuhi mjini kiev kati ya wajumbe kutoka pande zote mbili umezaa matunda.

Hapo jana Ukraine ilitia saini makubaliano yake ya kwanza lakini kisha baadaye kuweka masharti,hatua iliyoifanya Urusi kuyatangaza makubaliano hayo kutokubalika tena. Waziri mkuu wa Ukraine Bi.Tymoshenko

"Ukraine imekuwa mshirika wa kupitia usafirisha gesi kuelekea mataifa ya umoja wa ulaya."

Urusi huzalisha karibu robo ya gesi asili katika umoja wa ulaya na asilimia 80 ya gesi hiyo husafirishwa kupitia mabomba ya Ukraine. Mzozo kati ya mataifa hayo mawili ulikuwa umetokea wakati ambapo mataifa kadhaa ya bara hilo yakabiliwa na majira ya kibaridi kikali kuwahi kushudiwa katika muda wa miongo kadhaa.

Mataifa 12 wanachama wa umoja wa ulaya na mengine matano ambayo ni jirani ya mataifa yaliyo katika umoja huo yamekabiliwa na upungufu wa gesi tangu kampuni ya Gazprom nchini Urusi kufunga mabomba yanayopitisha gesi kupitia Ukraine. Mzozo huo ulitokana na kutoelewana kwa mataifa hayo mawili kuhusu mikataba na madai ya Ukraine kushindwa kulipa madeni yake.

Taifa jipya katika umoja wa ulaya Bulgaria ni mojawapo ya yale yaliathiriwa zaidi,huku Serbia ikitegemea gesi ya dharura kutoka Hungary na ujerumani.

Umoja wa ulaya tayari umewapeleka wachunguzi wake katika mabomba makuu ya kusafirisha gesi inayonuiwa kwa mataifa ya bara la ulaya kutoka Urussi kupitia Ukraine.

Kibarua chao ni kuhakikisha kuwa Ukraine haiibi tena gesi yeyote inayopitia katika mabomba hayo,madai ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na Moscow na kupigwa vikali na kiev.Itachukua kiasi cha siku tatu kwa hali kurejea kawaida ya usafairishaji gesi katika mataifa ya bara la ulaya.

Kufanikiwa kwa Urusi,kushawishi umoja wa ulaya kutatua mzozo kati yake na Ukraine na pia awali mzozo wake mwingine na Geogia ni ishara kuwa Moscow inapewa nafasi ya kwanza katika kutoa utatuzi wa mizozo na mataifa jirani zake.

Huku Ukraine ikiwa mbali na lengo lake la kujiunga na umoja wa ulaya kutokana na mzozo wake wa sasa, Umoja wa ulaya unaendelea kuwa mshirika mkubwa katika kutatua matatizo ya mataifa jirani yaliyo mashariki mwa bara la ulaya ,kuanzia mzozo wa sasa wa gesi na juhudi za kukabiliana na uhalifu katika mpka wa Ukraine na Moldova.