1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Havana: Kiongozi wa Cuba, Fidel Castro, anajihisi mzima zaidi.

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNq

Kiongozi wa Cuba, Fidel Castro, amesema anajihisi ana nguvu zaidi tangu alipoanza kuumwa July mwaka jana. Katika mazungumzo ya simu na rais wa Venezuela, Hugo Chavez, Fidel Castro alisema anajihisi ana nguvu zaidi. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 hajatoa hotuba tangu kufanyiwa operesheni mwaka jana, na amewahimiza wale walio na wasiwasi kuhusu hali yake ya afya wawe na subira. Kiongozi huyo wa Cuba alikabidhi madaraka kwa ndugu yake, Raul Castro, aliye na umri wa miaka 75, mwaka jana huku akipumzika baada ya kufanyiwa operesheni.