1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Infantino aanza kazi kama rais mpya wa FIFA

29 Februari 2016

Gianni Infantino ameanza kutekeleza majukumu yake kama rais mpya wa shirikisho la kandanda ulimwenguni – FIFA, ambapo shughuli yake ya kwanza rasmi ilikuwa ni kuzindua jumba jipya la makumbusho ya kandanda

https://p.dw.com/p/1I4MB
Schweiz FIFA Gianni Infantino
Picha: picture-alliance/dpa/E. Leanza

Infantino amesisitiza kuwa utekelezwaji wa mageuzi mapana yaliyoidhinishwa Ijumaa wiki iliyopita katika mkutano mkuu wa FIFA, ni jambo atakalolipa kipau mbele.

Jumba hilo la makumbusho mjini Zurich, limejengwa katika eneo la mita 3,000 za mraba na FIFA imesema litakuwa na karibu vitu 1,000, picha 1,400, video 500 na skrini 60 zitakazowekwa kwenye maonyesho. Infantino anasema jumba hilo linasherehekea mafanikio ya kandanda "Tunaweza kuona kuwa kitu cha muhimu katika kandanda ni rangi na jezi za timu na sio kingine. Ni vizuri sana na tunaweza kuona historia ya kandanda la ulimwengu kutoka mabara yote – kutoka kila sehemu. Inapendeza na kuigusa mioyo na nadhani ni muhimu kuwa tuna jumba hili.

Rais huyo mpya wa FIFA amesema hakuna haraka ya kumteua katibu mkuu, ambaye alisema katika kampeni yake ya urais kuwa atatoka nje ya bara la Ulaya.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Mohammed Khelef