1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran haitojadiliana na Umoja wa Ulaya

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJiN

TEHERAN:

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amesema,hakutofanywa majadiliano mapya pamoja na Umoja wa Ulaya kuhusu mradi wake wa nyuklia.Baada ya kukutana na baraza la mawaziri wake mjini Teheran,Ahmedinejad alisema,Iran katika siku zijazo itazungumza tu na Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA.

Ametamka hayo siku tatu baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa sababu ya nchi hiyo kukataa kusitisha harakati za kurutubisha madini ya uranium.Muda mfupi baada ya azimio hilo kupitishwa mjini New York,baadhi ya madola makuu yalitoa mwito kwa mrartibu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Javier Solana,kuanzisha majadiliano pamoja na mpatanishi wa Iran kuhusu mradi wa nyuklia wa nchi hiyo.Nchi nyingi za Magharibi zina wasiwasi kuwa Iran inajaribu kutengeneza silaha za nyuklia kwa siri.Teheran lakini imekanusha tuhuma hizo na inashikilia kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu.