1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Benazir Bhutto kujadiliana na viongozi wa upinzani

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79O

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan,Benazir Bhutto amewasili Islamabad kujadiliana na viongozi wa upinzani,lakini amefutilia mbali kukutana na Rais Jemadari Pervez Musharraf.Bhutto ameungana na Jaji Mkuu alieachishwa kazi,Iftikhar Chaudhry kutoa mwito kwa umma kufanya maandamano bila ya kujali polisi,mpaka amri ya hali ya hatari itakapoondoshwa.