1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Safishasafisha ya wanajeshi wa Pakistan kwenye msikiti wa Lal Masjid yamalizika

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjb

Vikosi vya usalama nchini Pakistan vimekamilisha opresheni ya safishasafisha katika msikiti wa lal Masjid mjini Islamabad.

Hata hivyo bado kuna taarifa za kutatanisha juu ya idadi kamili ya watu waliouwawa kwenye mapambano baina ya wanajeshi na wapiganaji wenye itikadi kali.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya ulinzi wapiganaji 73 na wanajeshi kumi waliuwawa kwenye mapambano hayo yaliyochukua muda wa zaidi ya siku nane.

Taarifa nyingine zinasema watu 106 wameuwawa katika ghasia hizo.

Hadi sasa hakujatolewa ripoti rasmi juu ya hatma ya mamia ya wanawake na watoto walioaminika kushikiliwa ndani ya msikiti huo. Inaaminika mashambulio zaidi ya kulipiza kisasi nchini Pakistan huenda yakashuhudiwa hasa baada ya kiongozi nambari mbili katika mtandao wa kigaidi wa alqaeda Ayman al Zawahiri kuwatolea mwito wa Pakistan kulipiza kisasi dhidi ya rais Pervez Musharraf.