1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Javier Solana akutana na mpatanishi wa Iran Saeed Jalili

30 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CVGQ

Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya,Javier Solana amekutana na Saeed Jalili ambae ni mpatanishi wa Iran kuhusika na mradi wa nyuklia wa nchi hiyo.Ripoti ya majadiliano hayo na ya Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa-IAEA zitaamua iwapo Marekani na washirika wake washinikize kuiwekea Iran vikwazo zaidi.

Serikali ya Tehran inashinikizwa kusitisha urutubishaji wa uranium,huku baadhi ya nchi za magharibi zikiwa na hofu kuwa inataka kutengeneza silaha za nyuklia.Iran lakini inasisitiza kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani tu.