1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, wanasoka wa kike wanapata mikataba inayowafaidi?

11 Desemba 2023

Soka la wanawake linatazamiwa kuwa tasnia itakayoleta mabilioni ya dola kwa mara ya kwanza katika historia yake. Hata hivyo ukuaji wa haraka wa mchezo una changamoto kadhaa ambayo wachezaji wanaweza wanapitia.

https://p.dw.com/p/4a1wl
England Super League Arsenal gegen Chelsea – Barclays Women Steph Catley in Aktion in London
Ligi kuu ya wanawake England, Arsenal dhidi ya Chelsea. pichani mwenye jezi nyekundu ni Steph Catley mchezaji wa klabu ya Arsenal.Picha: Daniela Porcelli/SPP/IMAGO

Soka la wanawake limepiga hatua kwa kasi sana na kufikia wakati mashabiki 59,402 wanalipa kutazama mechi ya soka ya wanawake. Moja ya mechi zilizopata mashabiki wengi zaidi ni pambano la Ligi Kuu ya Wanawake kati ya Arsenal na Chelsea katikati ya Desemba Mjini London. Lakini hali hii imetokea na inaendelea kutokea Australia, Marekani na mataifa kadhaa ya Ulaya.

Soma pia: Kombe la Dunia la Wanawake limevutia wengi

Kujitokeza wa wingi kwa mashabiki kwa namna hii ni dhibitisho zaidi ya kukua kwa kasi kwa michezo ya wanawake, ikichochewa na kandanda zaidi ya yote. Ripoti ya hivi majuzi ya kampuni ya uhasibu ya Deloitte ilitabiri kuwa michezo ya wanawake ingevuka kikomo cha mapato ya kimataifa cha $1 bilioni (€928 milioni) mnamo 2024 kwa mara ya kwanza, na kandanda ikifikisha dola milioni 555.

Lakini ukuaji huo wa kasi umeibua maswali muhimu kuhusu gharama yake kwa chama cha wachezaji FIFPRO, ambao walitoa ripoti yao wenyewe kuhusu Kombe la Dunia la 2023 nchini Australia na New Zealand siku hiyo hiyo. Ilifichua kuwa wachezaji, ambao athari zao katika kukuza mchezo zilionekana wazi uwanjani, kwenye viwanja na kwenye vibanda vya kuuza bidhaa, huenda wanapitia wakati mgumu.

Ripoti hiyo ilichunguza wachezaji 260 kutoka timu 26 kati ya 32 na kugundua kuwa mmoja kati ya watatu anapata chini ya dola 30,000 kwa mwaka kutokana na soka (bila kujumuisha marupurupu ya FIFA ya Kombe la Dunia), na mmoja kati ya watano anahitaji kibarua cha kujikimu.

Kibarua kigumu

Frauen Fußball Weltmeisterschaft | 2023
Kombe la Dunia la kandanda la wanawake.Picha: Ane Frosaker/SPP/IMAGO

Ingawa mabadiliko ni ya hivi majuzi, wale walio kwenye uwanja wa London, na katika Ligi kuu za wanawake kwa ujumla, wana taaluma kamili. Lakini ndivyo ilivyo katika ligi chache ulimwenguni, na hata wakati huo, wachezaji wanalipwa vizuri kwenye vilabu maarufu pekee. Hata huko, hali si kamilifu, na theluthi-mbili ya wachezaji wanakiri kuwa walikosa kufikia kilele cha viwango bora kimwili. Wachezaji kadhaa wa Arsenal walitinga hatua ya nne ya mwisho ya Kombe la Dunia nchini Australia na kisha wakakabiliana na mechi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wiki mbili baadaye.

Soma pia: Kombe la Dunia la Wanawake kuanza kutimua vumbi

Steph Catley alikuwa mmoja wao. Beki huyo aliongoza Australia katika mechi nne walipofikia hadi nusu fainali na alirejea kucheza mechi ya ushindani mjini London, mwendo wa saa 24 kwa ndege ugenini, siku 18 tu baada ya mchujo wa kuwania nafasi ya tatu. Kipindi cha kupona kilikuwa siku chache kwa wachezaji wa Arsenal wanaoichezeea timu ya kimataifa ya England.

"Kila mapumziko yanasubiriwa sana katika hatua hii," Catley aliiambia DW kuhusu mapumziko yajayo ya Krismasi katika ligi kuu ya wanawake. "Ni michezo mingi, hasa kuichezea Australia, ambapo tunafanya safari nyingi za ziada. Hilo ni jambo tunalopaswa kuwa makini nalo. Na ni jambo ambalo wafanyakazi wetu wa matibabu na makocha hufanya kazi nzuri sana ya kusimamia. Ni muhimu tu kujua mwili wako."

Wachezaji wazoefu kama Catley angalau hawahitaji kuweka usawa kati ya masomo au kibarua cha pili na taaluma zao za michezo na kufurahia ufikiaji wa miundombinu iliyoboreshwa ya matibabu na siha, hasa katika vilabu hivyo vinavyohusishwa na timu kuu za wanaume. Lakini hata kwao, madhara ya usafiri na mahitaji ya mechi yanaweza kuathiri haraka.

"Ikiwa wachezaji hawana kipindi salama cha angalau wiki tatu, au wiki tano, baada ya kampeni ndefu kabla ya kujiandaa kwa msimu, basi sio hatari tu kutoka kwa mtazamo wa kimwili na kisaikolojia lakini kwa mtazamo wa kiakili." alisema Mganga Mkuu wa FIFPRO Prof Dk. Vincent Gouttebarge.

Haikuwa hivyo kwa Alessia Russo, Catley, Lotte Wubben-Moy, Caitlin Foord, na wengine wengi katika ligi mbalimbali duniani, ambao walikuwa wamerejea kucheza mechi za hadhi ya juu, achilia mbali kufanya mazoezi na kusafiri, mara tu baada ya fainali. Kuanzishwa kwa Ligi ya Mataifa ya kandanda la wanawake mwaka huu kumeongeza zaidi idadi ya mechi kwenye kalenda ya wachezaji, na ndivyo pia mabadiliko yajayo ya Ligi kuu ya mabingwa Ulaya.

Kuimarika, lakini kwa gharama gani?

FIFA Fußball Frauen-WM | Finale Spanien vs England
Fainali ya Kombe la Dunia Wanawake kati ya Uhispania na England. Pichani ni Olga Carmona wa Uhispania na Alessia Russo wa England.Picha: Mathias Bergeld/Bildbyran/IMAGO

Ushahidi wa matakwa hayo ulikuwepo katika mchezo wa London derby. Mfungaji wa bao la kwanza la Arsenal, Beth Mead, alikosa Kombe la Dunia kutokana na jeraha la goti ambalo limekuwa changamoto kwa mchezo wa wanawake huku mchezaji mwenzake na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Leah Williamson akiwa bado hajapona jeraha hilo. Mrithi wa Williamson kama nahodha wa Uingereza Millie Bright, alikosa mchezo wa derby na maandalizi ya Kombe la Dunia baada ya kuwa mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi barani Ulaya msimu wa 2021-22.

"Ratiba zetu zinahitajika zaidi sasa," aliiambia DW mapema mwaka huu, kabla ya Kombe la Dunia. "Tunatarajiwa kufanya mashindano baada ya mashindano baada ya mashindano huku tukishindana kwa kila kombe unapocheza katika vilabu. Haiwezekani kuendelea na sisi sio roboti, miili yetu itaharibika," aliongeza.

Ripoti hiyo ilikubali hatua kubwa iliyofikiwa katika kilele cha mchezo wa wanawake, huku hali ya usawa wa kijinsia kwenye malazi, usafiri, na wafanyakazi wa usaidizi wakijadiliwa kwa ajili ya Kombe la Dunia na pesa zaidi zikiingia kwenye mchezo.

Soma pia: Waamuzi wa kike Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza

Lakini kama kampuni ya Deloitte ilivyosema: "Kuongezeka huku kwa ushiriki wa mashabiki na wawekezaji kunasababisha fursa mpya na kuboreshwa kwa vilabu na ligi, ikiwa ni pamoja na ushirikiano mkubwa wa kibiashara, kuongezeka kwa ushiriki na siku kubwa za mechi. Ili kuhakikisha ukuaji huu unaendelea kuwa thabiti na endelevu, mashirika ya michezo lazima yahakikishe kuwa uwekezaji unaelekezwa kwa maeneo sahihi, kama vile kuhimiza uaminifu wa mashabiki, ustawi wa wachezaji na kudumisha ushindani katika ligi."

Soka la wanawake, katika kiwango cha juu, sasa iko katika njia panda: kukua katika jinsi mchezo wa wanaume ulivyo, na pesa kama kigezo kikuu au kwenda polepole kidogo na kuwaangalia wale walioufanya mchezo huo kuwa wa kuvutia.

 

https://p.dw.com/p/4ZzVB