1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jinsi kugawana pato la mafuta Tanzania ?

27 Februari 2008

Tanzania bara na visiwani zinasaka njia ya kugawana mapato kutoka mafuta.

https://p.dw.com/p/DEN4

Kwa muujibu wa gazeti la THE East African linalochapishwa nchini Kenya, Tanzania inasaka sasa njia ya jinsi ya kugawana pato kutoka mafuta yaliogunduliwa karibuni nchini Tanzania kati ya Tanzania-bara na Zanzibar.

Kwani, kwa muujibu wa katiba ya muungano Tanzania-bara na Zanzibar zinabidi kuongoza kwa pamoja maswali yote yanayohusiana na mafuta yaliogunduliwa Tanzania.Visima vyene akiba kubwa ya gesi vimegunduliwa nje ya pwani ya Songo songo na Mnazi Bay.

Kwa muujibu wa taarifa hizo, Tanzania inasaka kampuni la kimataifa litakaloweza kutunga mfumo wa kugawana mapato kutoka mavuno ya mafuta hayo.Wizara ya nishati na madini ya Tanzania imeshapokea maombi kutoka makampuni 10 ya kimataifa yaliotayari kufanya kazi hiyo.

Bw.Tahir Abdullah,mkurugenzi wa mipango katika wizara ya nishati kisiwani Zanzibar amenukuliwa kuliambia gazeti la “THE EAST AFRICAN” wiki iliopita kwamba hakuna mtu yeyote wakati huu anaweza kusema jinsi ya kugawana mapato hayo yatayotokana na mafuta…

Akasema zaidi na ninanukulu,

“Mavuno ya mafuta yapasa kuongozwa kwa hali ya uwazi kabisa,yatozwe ikodi ya kutosha na kulindwa ili yasitumiwe vibaya na kwa ufisadi.”

Mabingwa wanadai kutokana na kuwa kiwango cha rushua nchini kuwa bado cha juu sana ,serikali ya Tanzania itahitaji kuzuwia biashara ya magendo na hata kuzuwia kugeuka biashara haramu ya kibinafsi.

Na ili biashara ya mafuta nchini Tanzania kuleta nafuu katika uchumi wan chi hii na kunyanyua maisha ya watanzania wa kawaida ,mpango huo unapaswa kupendekeza kushirikisha utaratibu wa ukaguzi huru wa hesabu ,ungemkono ukaguzi wa mashirika ya ukaguzi yasio ya kiserikali na kutilia nguvu kuwa na vyombo huru vya habari.

Ili kurahisha utaratibu huo,yabidi pazingatiwe barabara kuanzisha mfuko wa fedha zinazotokana na mafuta utakoendeshwa kitaalamu. Mfuko wa aina hiyo utalinda wizi wa fedha za mapato ya mauzo ya mafuta hayo .

Kama ilivyo katika mfano wa mfumo wa Alaska,sehemu ya mapato linalotokana na mauzo ya mafuta ligawiwe moja kwa moja na kutiwa katika akiba za banki za kila mtanzania-wanadai mabingwa .

Tanzania ina pato lisilo ridhisha la dala 250 kwa mwaka kwa kila mwananchi,lakini pia ina mali-asili nyingi mfano wa dhahabu,almasi,uranium,makaa yam awe ,bauxite na soda ash.

Mjadala wa hadharani juu ya utoaji mafuta,utozaji kodi na jinsi ya kugawana mapato utafanyika baadae mwaka huu.Tanzania-bara na Zanzibar –kwa muujibu wa katiba ya muungano kuongoza pamoja maswali yote ya biashara ya mafuta ya petroli.

Maswali mengine ya muungano ni sarafu moja,jeshi na siasa ya nje.

Azma ya katiba hii ya muungano ni kurahisisha juhudi za kuijenga jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa njia ambayo itahakikisha raslimali za nchi hii na urithi wake zinaongozwa kwa njia ambayo itahifadhi na kutumikia masilahi ya wote-kwa muujibu isemavyo katiba hiyo.

Swali la mafuta limezusha balaa kubwa la kisiasa,vita vya kienyeji na utekajinyara katika Niger Delta nchini Nigeria,Kusini mwa Sudan na katika Bakisa Valley huko Afrika magharibi.

Kumekuwapo pia sauti visiwani Zanzibar zlizohoji iwapo mafuta ni swali la muungano.Na ikiwa ndio, vipi madini na raslimali nyengine ziliopo Tanzania ?

Makampuni ya India,Marekani na Ulaya yameshiriki kutafuta mafuta na gesi nchini Tanzania.

Nchi mbali mbali tangu katika ulimwengu wa viwanda ulioendelea hata nchi changa zinategemea mafuta yanayopatikana kwa uhakika na bila ya misukosuko.

Lakini, matumisi mabaya na kutogawana mavuno kutoka pato la mafuta hayo ipasavyo mara kwa mara kuliongoza katik machafuko ya kijamii nay a kisiasa na baadhi ya wakati hata vita.Kwahivyo, kila pakiwapo ushirikiano na maridhiano makubwa na wananchi pamoja na uwazi wa jinsi mapto kutoka zao hilo yanavyotumiwa,ndipo mzalishaji mafuta kama inavyotazamiwa Tanzania atabakia imara na wa kutegemeka.

Tanzania karibuni hivi ilichimba visima 12 kusaka mafuta vikikadiriwa kuwa na akiba nzuri kabisa tangu ya gesi hata ya petroli.

Visima vikubwa vya gesi vimegunduliwa katika mwambao wa pwani ya songo Songo na Mnazi Bay.Akiba ya sasa ya gesi inakisiwa kuwa Cubic feet trillion.

Akiba ya sasa pekee ya gesi kutoka Songo songo kwa mradi wa umeme tayari ina soko la viwanda 17 muhimu vya matumizi ya gesi katika eneo la Dar-es-salaam.