1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Tutu ashutumu mpango wa UKIMWI

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTy

Askofu Mkuu Desmond Tutu ameishambulia vikali serikali ya Afrika Kusini hapo jana kwa kuchelewa kuanzisha mpango wa matibabu ya virusi vya HIV na UKIMWI na kusema kwamba maoni ya imani isio sahihi ya viongozi wa nchi hiyo yamesababisha vifo visivyo vya lazima.

Akiwakumbuka mashujaa waliokufa wakipiga vita utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel amesema watakuwa wamefadhaishwa kutokana na uharibifu uliosababishwa na janga la virusi vya HIV na UKIMWI ambapo amesema limekuwa likiuuwa watu 900 kila siku nchini humo.

Amesema wangelifurahi ingelikuwa kuna mpango ulio na uhalisi zaidi lakini wangelisikitika kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekufa kwa sababu ya kupewa kipau mbele kwa nadharia za maajabu.