1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Rais Karzai akutana na viongozi wa Taliban

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBp

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, amesema amekuwa akifanya mazungumzo na wanachama wa kundi la Taliban kujaribu kutafuta njia za kurejesha amani nchini humo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kabul, rais Karzai alisema mikutano yake na viongozi wa Taliban imekuwa ikendelea kwa muda mrefu.

Alisema yuko tayari kuzungumza na Taliban wote wa Afghanistan pamoja na kiongozi wa kundi hilo, Mullah Mohamed Omar, kuhusu njia za kumaliza mapigano nchini humo.

Wakati haya yakirifiwa, imethibitishwa kwamba wafanyakazi wawili wa kutoa misaada ya kiutu raia wa Ufaransa ambao walipotea wiki iliyopita, walitekwa nyara na wanamgambo wa Taliban kusini magharibi mwa Afghanistan na kupelekwa mkoani Helmand.