1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Taleban wafurushwa baada ya jaribio la kumteka afisa wa polisi.

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvp

Wapiganaji sita wa Taliban wameuwawa wakati wakijaribu kumkamata afisa wa polisi katika jimbo la kusini mashariki la Paktia.

Wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan imesema polisi na wanajeshi wamewazuwia wapiganaji hao na kuwafukuza baada ya kushambulia nyumba ya afisa huyo siku ya Alhamis usiku.

Kiasi cha kilometa 100 mashariki ya mji mkuu Kabul, mwanajeshi mmoja wa jeshi la NATO ameuwawa wakati bomu lililotegwa kando ya barabara lilipolipua gari moja ya jeshi hilo la kimataifa.