1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Maafisa 5 wa kijeshi wauwawa

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMZ

Maafisa watano wa polisi wameuwawa nchini Afghanstan baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujiripua karibu na msafara wa polisi kwenye mkoa wa Kandahar kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Maafisa wengine watatu walijeruhiwa katika tukio lililotokea nje ya makao makuu ya polisi kwenye mji wa Spin Boldak.Mapema hapo jana zaidi ya watu 32 waliuwawa wakati mabasi mawili yalipogongana katika barabara inayounganisha mji mkuu Kabul na Kandahar.

Kwa mujibu wa polisi mabasi hayo mawili yalikuwa yakisafiri kwa mwendo wa kasi.Kiasi cha abiria 30 walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.