1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Muda wa mwisho kwa mateka waongezwa kwa saa 24

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfm

Kundi la Taleban limeongeza saa 24 kama muda wa mwisho wa madai kutimizwa huku wakiendelea kuwazuilia mateka 23 wa Korea Kusini.Kundi hilo linatisha kuwaua watu hao endapo Korea Kusini haitaondoa majeshi yake yapatayo 200 nchini Afghanistan.

Kundi hilo la Taleban aidha linataka serikali ya Afghanistan kuwaachia wafungwa wao 10 na kujadiliana moja kwa moja na wawakilishi wa serikali ya Korea Kusini.Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea ili kushawishi kundi hilo kuwaachia mateka wa Korea Kusini.Kundi la Taleban linatisha kuwaua mateka hao ifikapo leo jioni endapo madai yao hayatatimizwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier anatoa tena wito wa kuachiwa raia mmoja wa Ujerumani ambaye bado anazuiliwa na kundi la Taleban nchini Afghanistan.Mwili wa Mjerumani wa pili aliyetekwa wiki jana unatarajiwa kuwasili nchini hapo kesho.Wizara ya mambo ya nje inathibitisha kuwa mwili huo ulikuwa na majeraha ya risasi japo chanzo cha kifo bado hakijulikani.