1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Maelfu kukabiliwa na janga la njaa

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gx

Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa na kundi la kutowa misaada la Oxfam wameonya hapo jana kwamba maelfu ya wananchi wa Uganada walioathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni watakabiliwa na janga la njaa kwa miezi kadhaa iwapo hawatoongezewa misaada.

Mkuu wa shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP Josette Sheeran amesema katika taarifa kwamba hali ni mbaya kwa mamia kwa maelfu ya watu ambao wamepoteza makaazi yao,mali zao na takriban mazao yao yote.

Kwa mujibu wa WFP mikoa ya kaskazini mashariki mwa Uganda imeharibiwa vibaya na mvua kubwa na mafuriko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa kwa miongo mingi ambapo watu wapatao 30,000 wamepotezewa makaazi au mazao yao kuharibiwa.