1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Mkutano kutenzua mgogoro wa mpakani

25 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBW3

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,Mbusa Nyamwisi amewasili nchini Uganda kufanya matayarisho ya mkutano wa kilele kati ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Joseph Kabila wa Kongo.

Mkutano kati ya majirani wawili unatazamiwa kufanywa juma lijalo ama nchini Uganda,Tanzania au Afrika ya Kusini.Azma ya majadiliano hayo ni kutenzua mgogoro wa mpakani,unaohusika na eneo la magharibi ya Uganda ambako kumegunduliwa mafuta mengi.