1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu mkuu wa UN alaani mauaji ya raia Palestina na Israel

28 Februari 2008

-

https://p.dw.com/p/DEdx

NEW-YORK

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumzia wasiwasi wake juu ya kuzidi kwa ghasia katika ukanda wa Gaza na kusini mwa Israel ambako raia wasio na hatia wanauwawa.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amesema hata hivyo anamatumaini kwamba hali hiyo haitazorotesha mpango wa amani wa mashariki ya kati.Wapalestina 11 akiwemo mtoto mchanga wa miezi sita waliuwawa katika mashambulio ya mabomu ya Israel hapo jana huku mashambulio ya roketi ya wapalestina yakisababisha mtu mmoja kuuwawa.

Amelaani mauaji ya watoto wanne wakipalestina akiwemo huyo mchangakatika shambulio lililofanywa na wanajeshi wa Israel katika Gaza na kuitaka nchi hiyo kujizuia na matendo kama hayo na kuheshimu sheria ya kimataifa juu ya ubinadamu.Aidha amelaani mashambulio ya roketi ya wanamgambo wa Hamas na makundi mengine ya wanamgambo wa Kipalestina.