1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya imewataka wanadiplomasia wa kigeni kutoingilia siasa wakati wa uchaguzi

2 Februari 2007

Serikali ya Kenya imewataka wanadiplomasia wa kigeni kukoma kuingilia siasa za ndani ya nchi hiyo inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

https://p.dw.com/p/CHKt

Naibu waziri wa mambo ya nje nchini humo Moses Wetangula alitoa matamshi ya kuwaonya wanadiplomasia hao baada ya mwanadiplomasia wa Uingereza nchini Kenya Adam Wood kuitaka serikali kutowalazimisha wafanyikazi wa serikali kuipigia kura wakati wa uchaguzi.

Saumu Mwasimba alizungumza na Dkt.Noeh Wekesa ambaye ni waziri wa sayansi na technologia na vile vile rafiki wa karibu wa Bw. Wetangula.