1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Kujiuzulu kwa Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Moses Wetangula

27 Oktoba 2010

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Moses Wetangula, amesema kwamba anajiuzulu huku kukiweko madai ya ufisadi dhidi yake katika ishara za hivi karibuni za kupambana na jambo hilo.

https://p.dw.com/p/PqS6
Bunge la Kenya ambako mahojiano yaliendelea kuhusu mkasa wa waziri wa mambo ya kigeni Bw.WetangulaPicha: DW /Maya Dreyer

Bwana Wetangula alisema amefanya uamuzi wa kibinafsi wa kujiweka kando kama waziri wa mambo ya kigeni ili kutoa nafasi kwa wale wanaomuandama, na pia kutoa nafasi kwa uchunguzi ufanyike kutokana na tuhuma hizo. Alihakikisha kwamba atarejea katika baraza la mawaziri punde pale uchunguzi utkapokamilika, kwa vile anajua yeye hana makosa.

Punde hivi Othman Miraji alimuuliza kwa njia ya simu waziri mwenzake, Profesa Anyang' Nyong'o, wa huduma za afya, kuhusu hatua ya Moses Wetangula...

Mwandishi: Othman Miraji

Mpitiaji: Josephat Charo