1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenyatta na Raila washiriki maombi ya amani

25 Februari 2013

Wagombea wawili wanaopewa nafasi kubwa ya katika uchaguzi utakaofanyika Machi 4 mwaka huu nchini Kenya, wameshiriki katika sala ya kuliombea taifa hilo kufanya uchaguzi wa amani na utulivu na kupuka kuepuka vurugu

https://p.dw.com/p/17lQc
Kenya's Deputy Prime Minister and Jubilee Alliance Presidential candidate in the upcoming Presidential elections, Uhuru Kenyatta, addresses surpporters during a plotical rally in the capital Nairobi on February 13, 2013. Kenya's eight presidential candidates held the country's first ever face-to-face debate this week as tensions mount ahead of next month's election, five years after bloody violence erupted in the wake of the last vote. While two main candidates -- Uhuru Kenyatta and Raila Odinga -- dominate the race for the March 4 election, all the hopefuls have potential influence, especially if voting goes to a second round run-off. AFP PHOTO / SIMON MAINA (Photo credit should read SIMON MAINA/AFP/Getty Images)
Mgombea Uhuru KenyattaPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Wagombea hao wawili ambao ni Waziri mkuu wa sasa Raila Odinga, na Uhuru Kenyatta mtoto wa Rais wa kwanza wa nchi hiyo, wote walijiunga na maelfu ya raia wengine wa Kenya katika kuiombea Kenya iwe na uchaguzi wa amani na salama.

''Uchaguzi wa mwaka 2007 na machafuko yaliyofuatia sasa ni historia'' alisema Uhuru Kenyatta, ambaye aliamua kuingia kinyang'anyiro cha kumrithi rais anayeondoka Mwai Kibaki, licha ya kukabiliwa na kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusiana na tuhuma za vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu katika uchaguzi wa mwaka 2007. Watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha yao katika ghasia hizo, na wengine kadhaa kulazimika kuhama makazi yao.

Ahadi ya Raila Odinga

Katika sala hiyo bwana Kenyatta aliahidi Ninaahidi kuwa atahubiri amani muda wote. Kwa upande wake Raila Odinga, naye pia aliwataka wakenya kuweka mbele amani. ''Sote tunatakiwa kuhamasisha amani, hatuhitaji mapigano baina yetu, sisi wote ni wakenya, tuchague viongozi wetu kwa amani na utulivu´´ alisema Raila Odinga.

Kenya's Prime Minister Raila Odinga (C) waves alongside his Coalititon for Restoration of Democracy (CORD) alliance partners, his running mate Kalonzo Musyoka (L) of Wiper Democratic movement party and Moses Wetangula (R) of Ford party during a political rally in the coastal town of Malindi on February 9, 2013. Odinga, the presidential candidate for Coalition for Reforms and Democracy (CORD) and his running mate Kalonzo Musyoka campaigned in Mombasa and along Kenya's coast over the weekend in the build up to Kenya's general elections slated to be held on March 4, 2013. AFP PHOTO/ Will BOASE (Photo credit should read Will Boase/AFP/Getty Images)
Mgombea urais Raila OdingaPicha: Will Boase/AFP/Getty Images

Aidha, Odinga alisema kuwa machafuko ya mwaka 2007-2008 ambayo yalisababisha maelfu ya watu kuhama makazi yao, yalibadilisha mtazamo wa kisiasa, na kuharibu picha ya kenya ambayo ni muhimili wa amani katika ukanda huo.

Mwandishi: Hashim Gulana /AFP
Mhariri: Daniel Gakuba